
Mwenyekiti Zakaria Lazaro Lukumay amesema kwamba anaamini kwamba CCM ndicho chama pekee ambacho kinagusa maisha ya watanzania hivyo ameamua kujiunga ili kutetea, kulinda, na kusimamia rasilimali za nchi ikiwa ni pamoja na kupiga vita ufisadi, rushwa na mambo mengine yanayofanana na hayo.
Katika taarifa yake aliyoituma kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Siha, Lukumay ameongeza kuwa anaamini katika maamuzi yake aliyoyafanya atakuwa huru kuungana na Mh. Rais Magufuli katika kutekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM ya 2015 .
Mtazame hapa chini Diwani Lukumay akifunguka zaidi