Jumatatu , 13th Sep , 2021

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, amesema kwamba kwa hali inavyoendelea kwa sasa serikali itaendeshwa kwa matendo makali na si maneno makali na kwamba watendaji wa serikali wasitarajie kumuona yeye akiwafokea na badala yake atafoka kwa kalamu.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan

Kauli hiyo ameitoa leo Septemba 13, 2021, mara baada ya kukamilika kwa zoezi la kuwaapisha mawaziri wanne wa Wizara mbalimbali pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, aliowateua hapo jana na kuwaapisha leo katika Ikulu ya Chamwino Dodoma.

"Msinitegemee kwa maumbile yangu haya pengine na malezi yangu kukaa hapa na kufoka, nahisi si heshima, na kwa sababu nafanyakazi na watu wazima wanaojua jema na baya na kila mtu anajua afanye nini, msitegemee nitaanza kufoka hovyo hovyo, nitafoka kwa kalamu," amesema Rais Samia.