Ijumaa , 8th Jul , 2016

Maafisa watano wa polisi mjini Dallas, Marekani wamepigwa risasi na kuuawa wakati wa maandamano ya kupinga mauaji ya watu weusi. Maafisa wengine sita wanauguza majeraha.

Polisi wakiwa katika hali ya kujihami kufuatia maandamano ya kupinga mauaji ya watu weusi jimbo la Dallas Marekani.

Mauaji ya polisi yamefuatia kuuawa kwa wamarekani wenye asili ya weusi ambapo Raia wa Louisiana Marekani walianzisha maandamano kupinga kitendo cha mauaji ya Wamarekani weusi Alton Sterling naPhilando Castile waliouawa kwa kupigwa risasi na polisi jambo ambalo limezua hasira katika maeneo mengi baada ya video ya mauaji kusambaa.

Maafisa wa polisi katika mji ulio katika jimbo la Texas, wamenasema mauaji ya polisi yametekelezwa na washambuliaji wawili wa kulenga shabaha.

Aidha Ufyatuaji risasi ulitokea mwendo wa saa tatu kasorobo usiku saa za Texas waandamanaji walipokuwa wakipitia barabara za mji na kuwafanya waandamanaji kukimbilia usalama wao.