Jumamosi , 18th Dec , 2021

Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Arusha, Mrakibu wa Polisi SP Solomoni Mwangamilo, amewaonya baadhi ya madereva wenye tabia ya kubashiri (Bet) kwa kushindana barabarani ili kuwahi kufika wanakokwenda na kuwataka kuacha mara moja tabia hiyo.

Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Arusha, Mrakibu wa Polisi SP Solomoni Mwangamilo

Kauli hiyo ameitoa hii leo Desemba 18, 2021, wakati jeshi hilo likifanya ukaguzi wa zaidi ya magari 100, na kutoa elimu kwa madereva na abiria wanaotumia vyombo vya moto kwenda mikoa mbalimbali hapa nchini.

Aidha, SP Mwangamilo amewasihi wananchi kutoa taarifa za madereva wanaokiuka sheria za usalama barabarani na kwenda mwendokasi ili kupunguza ajali ambazo zinaweza kuepukika.