
Jeshi la Polisi Mkoani Pwani limethibitisha kutokea kwa tukio la watu wawili kupoteza maisha papo hapo na mmoja kujeruhiwa vibaya mwilini baada ya kutokea kwa mlipuko unaodaiwa kutokana na chuma ambacho mmoja wao alikua anakikata kwenye Banda linalojihusisha uchomeleaji vyuma chakavu huko Mtaa wa Magomeni Wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Pwani Salim Morcase amesema tukio hilo limetokea jana Agosti 31 na kwamba mlipuko huo pia umeshababisha uharibifu wa nyumba kadhaa zilizopo jirani na ilipotokea mlipuko huo.
Amebainisha Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi wa kina Kwa kushirikiana na vyombo vingine vya usalama Ili kubaini chanzo Cha mlipuko huo na ni wa kitu gani kisha taarifa kamili itatolewa mapema iwezekanavyo.