Magereza wajawazito wanapewa udongo

Jumatano , 17th Apr , 2019

Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Kangi Lugola amefafanua kwamba wafungwa wanaokuwa wajawazito ndani ya magereza ya Tanzania, huwa wanasaidiwa kupata huduma muhimu kulingana na mahitaji yao ya kiafya.

Kangi Lugola

Akijibu swali la Mbunge Farihiya aliyetaka kujua namna magereza inavyowasaidia wajawazito pindi wanapohitaji haswa kipindi wanapopata uchungu wa kujifungia.

"Kwenye jeshi la magereza tunazo zahanati na huduma za Afya, Wanawake wanahudhuria klinic, na hata mahitaji yote mjamzito anayohitaji magereza yanapatikana.

Katika kuongezea msisitizo, Waziri Lugola amesema kwamba,"vyakula vya wajawazito vipo na hata vile vitu vya kusisimua hata kama ni udongo wanapatiwa.