
Lengai Ole Sabaya
Hukumu ya leo inatarajiwa kuamua hatima ya kiongozi huyo wa zamani na wenzake endapo wataachiwa huru, kwa kuwa baada ya kesi hii hawana nyingine iliyosalia mahakamani.
Katika kesi ya kwanza Sabaya na wenzake wawili walihukumiwa kifungo cha miaka 30 jela, hukumu ambayo Mei 6, 2022 ilitenguliwa na Mahakama Kuu na kuwaachia huru baada ya kubaini dosari zilizojitokeza katika mwenendo wa kesi ya msingi katika mahakama ya chini.