
Kikao cha Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya makazi na watumishi wake
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. Angelina Mabula amesema hayo katika kikao kazi kilichofanyika Dar es Salaam na makamishina wa ardhi nchi nzima kujadili njia ya kupitia kama Wizara kufuatia malalamiko ya wadau wa Sekta ya ardhi Kwa vikao vilivyohitimishwa hivi majuzi na wadau wa Sekta ya Milki na wengine.
Waziri Mabula amesema makamishna ambao wamebainika kusababisha migogoro ya ardhi wachukuliwe hatua za kisheria huku katibu mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Allan Kijazi akisema kuanzia sasa wataanza kusainisha mikataba maalum na watendaji wizarani hapo ili kuweka dhamana ya usimamizi ikilenga sasa kuwajibishana Kwa watendaji wazembe wanaosababisha migogoro mingi.
Kadhalika, suala la ukusanyaji mapato limetajwa kutoridhisha kutokana na uzembe wa watendaji ambao wameshindwa kuzingatia upangaji wa miji, utoaji wa vibali usiofata mipango miji na akiwataka sasa kuzingatia sheria.
Pia Waziri wa Ardhi nyumba na maendeleo ya makazi ameagiza kuchukuliwa hatua kwa watendaji Kwenye sekta hiyo wanaotoa vibali vya vituo vya mafuta holela nje ya utaratibu.