Jumatano , 16th Nov , 2022

Makamu wa Rais wa Tanzania, Dk. Philip Mpango ametoa maagizo  kumi kwa Wizara za kisekta ili kukabiliana na tatizo la uhaba wa maji nchini

Maagizo hayo yapo kupanda miti rafiki wa maji kwenye vyanzo na kushusha bei ya gesi ya kupikia   ili wananchi waachane na matumizi ya mkaa ambao unachangia uharibifu wa mazingira

Dkt. Mpango ametoa  maagizo hayo  kwenye mkutano wa nane wa Mwaka Bodi za Maji za Mabonde  unaofanyika kitaifa jijini Mbeya  pamoja na uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti rafiki wa maji kwenye vyanzo.

Waziri wa Maji, Juma Aweso, amesema  shughuli za kibinadamu kama vile kilimo, uchomaji mkaa zimechangia kwa kiasi kikubwa kuharibu vyanzo vya   maji huku Spika wa Bunge la Tanzania ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mbeya mjini, akibainisha haya.

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, TAMISEMI, David Silinde amesema wakuu wa Mikoa yote nchini wanapaswa kuandaa mpango kazi wa upandaji miti rafiki wa vyanzo vya maji  kwenye maeneo yao  na taarifa hiyo wapatiwe.