Jumanne , 25th Jan , 2022

Jeshi la Polisi Kanda Malum ya Dar es Salaam, linawashikilia watu wawili kwa tuhuma za mauaji ya mwanamke aitwaye Barke Rashid, aliyeuawa Januari Mosi, 2022, akiwa guest maeneo ya Tabata, ambapo mmoja amekiri kutekeleza unyama huo baada ya kuahidiwa kiasi cha shilingi milioni 1.7.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro, kulia ni Barke Rashid aliyeuawa

Taarifa hiyo imetolewa leo Januari 27, 2022, na Kamanda wa Polisi wa Kanda hiyo Jumanne Muliro, na kusema chanzo cha mauaji hayo ni kwamba watuhumiwa waliokamatwa mmoja wao alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na marehemu na kwamba licha ya kumhudumia bado hakuridhika na aliendelea na mahusiano na wanaume wengine.

"Chanzo cha mauaji haya kwa mujibu wa uchunguzi wa awali inadaiwa mtuhumiwa Charles Gregory au White, alikuwa ni mpenzi wa marehemu na alikuwa anadai amemgharamia sana ikiwa ni pamoja na kumpangishia nyumba na kudai marehemu alikuwa na mahusiano na wanaume wengine," amesema Kamanda Muliro.

Aidha Kamanda Muliro ameongeza kuwa uchunguzi wa kina juu ya tukio hilo bado unaendelea na watuhumiuwa watafikishwa mahakamani.