
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa William Lukuvi.
Kauli hiyo imetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi alipokutana na madalali wa nyumba na ardhi pamoja na wadau wa nyumba nchini, lengo likiwa ni kuwapa utaratibu wa uuzaji wa dhamana unaofanywa na mkopeshaji endapo mkopaji ameshindwa kulipa deni.
Mhe. Lukuvi pia amekemea viongozi wenye mamlaka za kusimamia ardhi wanaoshirikiana na maafisa wa benki kupanga njama za kujiuzia ardhi kwa bei rahisi na kupoteza haki za watanzania.
Ameongeza kuwa kazi kubwa ya madalali ni kutekeleza amri zilizotolewa na mabaraza kama zilivyo, ila changamoto ni kwamba madalali walio wengi huwa wanafanya kinyume na maelekezo waliyopewa.
Kwa sasa ufuatiliaji wa mwenendo wa madalali umekuwa mgumu kutokana na kukosekana kwa kanuni za maadili ya kazi zao kama ambazo zinatumika na idara ya mahakama nchini hivyo inakuwa vigumu kuwajibisha madalali kwa kukiuka maadili ya kazi zao.
Amewataka wananchi kuwa makini na wimbi la madalali wasio waaminifu kwani watawaibia fedha zao.