
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja
Hatua hiyo ni kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan za kutangaza utalii kupitia filamu ya Royal Tour.
"Lazima kila mwezi tuwe na tukio la kiutalii jijini Dar es Salaam na tufanye kwa kushirikiana," amesema Naibu Waziri Masanja.
Aidha, amesema ni jukumu la kila taasisi kuhakikisha inatangaza vivutio vyote bila kubagua taasisi nyingine.
Amewataka maafisa hao kutenga bajeti za kutangaza vivutio vya utalii vya maeneo yao ya kazi kupitia vipeperushi na kuviweka katika maeneo yanayotembelewa na wageni.
Sambamba na hilo amezitaka taasisi za Wizara hiyo kuitumia fursa ya meli inayoleta watalii nchini kwa kutangaza ujio wake kwa kualika waongoza watalii kushiriki katika kuwapokea na kuwatembeza katika vivutio mbalimbali vilivyoko jijini Dar es Salaam.