Jumapili , 22nd Sep , 2019

Eneo la starehe (Pub) lililoko kwenye ufukwe wa Coco Beach jijini Dar es salaam, limetekea kwa moto huku chanzo cha moto, kikiwa bado hakijajulikana.

Eneo hilo ambalo lipo Msasani jijini Dar es salaam linatajwa kuanza kuungua kwa moto, majira ya saa 7 mchana, ambapo kwa mujibu wa Meneja Pub hiyo, Davis Urasa mpaka sasa bado hawajatanbua hasara kiasi gani iliyotokea.

"Kama mnavyoona kuna moto umetokea hapa na ulianza majira ya saa 7 mchana, na tulianza kuona moshi ukitokea juu baada ya hapo muhusika wa umeme alijaribu kwenda kuzima, japo hatukufanikiwa" amesema Meneja Davis urasa

"Mpaka sasa kiundani bado hatujajua chanzo ni nini, tunasubiri taarifa kutoka kwa Polisi wajaribu kutueleza" amesema Meneja wa Pub hiyo Samia Rajab

Akizungumza na EATV / EA Radio Digital Kamanda wa Polisi  Mussa Taibu, amesema na wao wamepokea taarifa hizo na wamefanya juhudi za awali za kuhakikisha moto huo unazimwa, na sasa wanafuatilia chanzo ni nini.

Tazama video hapo chini