Alhamisi , 13th Oct , 2022

Nchi ishirini na sita za Afrika zimepiga kura kuunga mkono azimio la Umoja wa Mataifa la kukataa kura ya maoni yenye utata ya Moscow katika maeneo manne ya Ukraine ambayo ilitangaza kuwa sehemu ya Urusi. 

Nchi kumi na tisa hazikushiriki  ikiwa ni pamoja na Eritrea ambayo hapo awali ilipiga kura kukataa azimio la Umoja wa Mataifa la kulaani uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.

Washirika wanaotambulika wa Urusi, ikiwa ni pamoja na Mali, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Ethiopia, Jamhuri ya Congo, Afrika Kusini, Sudan, Uganda na Zimbabwe pia ni miongoni mwa nchi nyingine za Afrika ambazo  hazikupiga kura.

Nchi tatu kati ya hizo zilimkaribisha mwanadiplomasia mkuu wa Urusi Sergei Lavrov alipozuru bara hili  mwezi Julai.