Jumatatu , 25th Jul , 2022

Halmashauri ya Jiji la Mbeya, imepewa miezi mitatu, kujenga mnara wa Mashujaa wa Tanzania waliofariki kwenye vita ya Pili ya Dunia mwaka 1939/1945 na kuandika majina ya mashujaa hao ili kuweka kumbukumbu sahihi.

Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Juma Homera

Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Juma Homera, ndiye aliyetoa agizo hilo wakati wa maadhimisho ya siku ya Mashujaa iliyofanyika eneo walipozikwa mashujaa hao ambapo maofisa mbalimbali wa serikali waliweka mashada kwenye makaburi hayo.

Katibu Tawala mkoa wa Mbeya, Dk. Angelina Lutambi, amesema siku ya mashujaa nchini inatoa nafasi ya kuwakumbuka na kuwaombea watu mbalimbali waliopoteza maisha.

Viongozi wa dini na wananchi wa Jiji la Mbeya wakapongeza hatua ya serikali kujenga mnara utakotambulisha majina ya mashujaa 36 waliofariki wakilipigania Taifa na mataifa mengine.