Jumatano , 5th Oct , 2016

Bodi ya wadhamini CUF imefungua maombi ya kufungua kesi katika Mahakama Kuu dhidi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi, Prof. Ibrahim Lipumba na Wanachama 12 waliosimamishwa uanachama wa chama hicho.

Prof Ibrahim Lipumba

Katika maombi hayo bodi hiyo inaomba kibali cha kufungua kesi dhidi ya msajili, Lipumba na wenzake ili mahakama itoe amri ya kumzuia Msajili asifanye kazi nje ya mipaka ya mamlaka yake kisheria

Jana wajumbe wanne wa bodi hiyo waliibuka na kuunga mkono msimamo wa Msajili wa Vyama vya Siasa na kupanga kuwakutanisha Prof. Lipumba na Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif ili kumaliza mgogoro wao.

Mgogoro wa CUF umeibuka mara tuu baada ya aliyekuwa mwenyekiti wake taifa Prof. Ibrahim Lipumba kutangaza adhma ya kutaka kurudi kwenye nafasi yake hiyo baada ya kutangaza kujiuzulu nyakati za uchaguzi mwishoni mwa mwaka jana kitendo kilichochochea mgongano ndani ya chama hicho.