Jumamosi , 11th Sep , 2021

Mratibu wa Programu ya Ongea na Vijana kutoka Tume ya Kudhibiti Ukimwi nchini (TACAIDS) Dkt. Pendo Saro, amesema kuwa utafiti walioufanya unaonesha kwamba mkoa wa Dodoma unaongoza kwa mabinti kufanya ngono wakiwa na umri mdogo.

Mratibu wa Programu ya Ongea na Vijana kutoka Tume ya Kudhibiti uUkimwi nchini (TACAIDS) Dkt. Pendo Saro.

Kauli hiyo ameitoa hii leo Septemba 11, 2021, jijini Dodoma, wakati wa uzinduzi wa programu ya Ongea Radio, kipindi ambacho kinachorushwa na East Africa Radio kila Jumamosi kuanzia saa 6:00- 6:30 mchana, chenye lengo la kutoa elimu kwa vijana walio katika umri wa balehe kubadili tabia zao na namna ya kujiepusha na maambukizi ya Ukimwi.

"Katika utafiti tuliofanya tumebaini mkoa wa Dodoma unaongoza kwa mabinti kufanya ngono wakiwa na umri mdogo, ukifuatiwa na mkoa wa Tabora," ameeleza Dkt. Pendo

Aidha Dkt. Pendo akaongeza kuwa, "Mkoa wa Iringa na Njombe, ndiyo mikoa ambayo mabinti wake wanauelewa wa kutosha kuhusu ngono wakiwa na umri mdogo".