Mo Dewji awekwa chini ya uangalizi

Jumatano , 6th Feb , 2019

Serikali imesema mashamba sita yanayomilikiwa na Mfanyabiashara Mohamed Dewji yapo chini ya uangalizi na iwapo atashindwa kutekeleza masharti watayafuta.

Mohamed Dewji

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi wakati akijibu hoja za wabunge walizozitoa katika mjadala wa taarifa ya kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii.

Ameeleza kwamba awali mfanyabiashara huyo alipewa onyo katika mashamba 12 kati ya 21 aliyokuwa akimiliki.

Aidha amesema Serikali tayari imefuta hati za mashamba sita na bado sita ambayo yapo kwenye uangalizi na kubainisha kuwa Tanzania ina mashamba makubwa 2000 ya kilimo na ufugaji.

Amefafanua kwamba kwa kipindi cha miaka mitatu wamefuta mashamba 46 katika maeneo mbalimbali ambayo yameshindwa kutimiza masharti.