Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora ACP Richard Abwao
Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora ACP Richard Abwao, amesema tukio hilo limetokana na imani za kishirikina ambapo mtuhumiwa amekuwa akisumbuliwa na tatizo la ugonjwa wa kifafa ambao amekuwa akiuhusisha kulogwa na baba yake mzazi .
Kamanda Abwao amesema mtuhumiwa huyo baada ya kutiwa nguvuni alihojiwa na kukili kutekeleza mauaji hayo ambapo kwa sasa zinafanyika taratibu za kumfikisha mahakamani.


