"Mtu asikujengee chumba cha kulala na mkeo" - JPM

Alhamisi , 26th Mar , 2020

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, amesema kuwa miongoni mwa makosa makubwa ambayo mtu anaweza kuyafanya ni pamoja na kumruhusu mtu wa nje kumjengea chumba cha kulala yeye na mke wake.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli.

Rais Magufuli ameyabainisha hayo leo Machi 26, 2020, mara baada ya kupokea taarifa maalum kutoka kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na TAKUKURU na kusema kuwa Mataifa mengi duniani, yamejitokeza kwa wingi yakitaka kuijenga Ikulu ya Chamwino Dodoma, huku malengo yake yeye Ikulu hiyo itajengwa na wazawa na itafanana na ile ya Dar es Salaam.

"Wakati tulipohamia hapa, wapo watu na Mataifa mengine walitamani watujengee Ikulu, lakini kosa kubwa ambalo mtu unaweza kulifanya ni kuruhusu mtu akujengee chumba chako ambacho utalala na mke wako, maana yake Ikulu ingekuwa wazi na mimi tangu nimekaa hapa kwa siku chache hapa ni pazuri sana" amesema Rais Magufuli.