Mwanamke wa miaka 21 TZ akutwa na Corona

Jumatatu , 30th Mar , 2020

Idadi ya wagonjwa walioambukizwa na Virusi vya Corona nchini Tanzania imeongezeka na kufikia 19, ambapo watatu kati ya walioongezeka ni kutoka Dar es Salaam na wawili kutoka Zanzibar.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu.

Taarifa hiyo imetolewa leo Machi 30, 2020, na Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu, ambapo amesema kuwa wagonjwa hao waliopatikana Dar es Salaam, yupo mwenye umri wa miaka 21 ambaye ni miongoni mwa watu waliokuwa wanafuatiliwa.

"Wa kwanza ni mwanaume mwenye umri wa miaka 49, ambaye alikutana na raia wa kigeni aliyetoka kwenye nchi zilizoathirika zaidi, mwingine ni mwanamke (21), aliyekuwa akifuatiliwa na watatu ni mwanaume (49), ambaye pia ni miongoni mwa wale waliokuwa wakifuatiliwa" imeeleza taarifa ya Waziri Ummy.

Aidha Waziri Ummy amesema kuwa wagonjwa wawili waliopatikana Zanzibar, taarifa zao zitatolewa na Waziri wa Afya wa Zanzibar.