Jumanne , 10th Dec , 2019

Mwili wa Mfanyabiashara Ali Mufuruki unaagwa leo Disemba 10, 2019 katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam, baada ya mwili wake kuwasili jana kutokea Afrika Kusini.

Marehemu Ali Mufuruki

Mufuruki amefariki Dunia usiku wa kuamkia Jumapili ya Disemba 08, 2019 akiwa Afrika Kusini, ambapo alikuwa akipatiwa matibabu ya maradhi yaliyokuwa yakimkabili katika Hospitali ya Morningside.

Viongozi mbalimbali wa Kitaifa na Wafanyabiashara wameshiriki kuaga kwa mwili wa Ali Mufuruki.

Watu mbalimbali walieleza kuguswa na kifo mfanyabiashara huyo, akiwemo Rais Magufuli ambaye alieleza msiba huo umemgusa sana.

Viongozi wengine walioeleza hisia zao kwa kifo cha Mfanyabiashara huyo ni Waziri Ummy Mwalimu, Zitto Kabwe.