Jumatatu , 17th Aug , 2015

Mgombea Urais kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, ambaye pia anawakilisha Umoja wa Katiba ya Wananchi UKAWA,Mh. Edward Lowassa amasema atawafikisha viongozi wa Serikali ICC ambao wanakiuka haki za binadamu.

Mgombea Urais kupitia chama cha Demekrasia na Maendeleo CHADEMA, ambae pia anawakilisha Umoja wa Katiba ya Wananchi UKAWA,Mh. Edward Lowassaa akihutubia Wananchi walijitokeza jijini Mwanza.

Lowassa amesema hayo jana wakati ikihutubia malefu ya wananchi waliojitokeza katika mkutano wa hadhara katika viwanja vya Furahisha jijini Mwanza na kuongeza kuwa jeshi la polisi linapaswa kutenda haki kwa vyama vyote na kuacha upendeleo wa kuwapiga wananchi bila sababu.

Hatua hiyo inakuja baada ya msafara wake uliokuwa ukiandama kwenda kumpokea uwanja wa ndege kupigwa mabomu ya machozi kwa kuwatawanya kwa kuwa jeshi la polisi lilikataza maandano yoyote wakati wa kumpokea kiongozi huyo.

Aidha Mh. Lowassa amewapongeza Wananchi wa Mwanza wa Kanda ya Ziwa kwa ujumla kwa kumpokea na kuahidi kuwa endapo atafanikiwa kuchaguliwa atatatu matatizo ya barabara,usafiri wa meli na Viwanda.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia ambaye ni Mwenyekiti mwenza wa Umoja wa Katiba ya Wananchi Mh. Freeman Mbowe amesema wamegundua kuna wanajeshi watalaamu wa IT. waliopelekwa tume ambapo amesema wamebaini wanataka kutumika kuhujumu Uchaguzi Mkuu.