
Papa Benedict aliongoza Kanisa Katoliki kwa muda usiozidi miaka minane hadi mwaka 2013, akawa Papa wa kwanza kujiuzulu tangu Gregory XII mnamo mwaka 1415
Benedict alitumia miaka yake ya mwisho katika monasteri ya Mater Ecclesiae ndani ya kuta za Vatican
Mrithi wake Papa Francis hivi karibuni alitangaza kuwa hali ya kiongozi huyo haikuwa nzuri na kulitaka Kanisa kumuombea ili afya yake irejee vizuri