Rais mwingine kumtembelea JPM kijijini kwake

Ijumaa , 12th Jul , 2019

Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, kesho, Julai 13 anatarajia kufanya ziara binafsi nchini Tanzania.

Ziara wilayani Chato

Katika ziara hiyo, Rais Museveni atamtembelea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli, Kijijini kwake Mlimani, wilayani Chato, mkoani Geita.

Akiwa kijijini hapo, Rais Museveni atafanya mazungumzo na mwenyeji wake Rais Magufuli. Ikumbukwe hivi karibuni Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta alimtembelea Rais Magufuli nyumbani kwake, ambapo alifanya mazungumzo naye binafsi.