Jumatatu , 20th Nov , 2023

Rais wa Kenya William Ruto amesema kuwa kwa sasa macho yake hayaelekei kuchaguliwa tena katika Uchaguzi Mkuu wa 2027, bali yanalenga kuleta mageuzi ya kudumu nchini Kenya.

Akizungumza wakati wa ibada katika kanisa la Sotik, Kaunti ya Bomet, Ruto alibainisha kuwa maslahi yake ni hasa katika kurekebisha mbinu ya utoaji huduma katika miongo kadhaa iliyopita kwa vizazi vya taifa hilo.
Ruto amewaonya viongozi ambao lengo kuu lao ni kupata nafasi zao katika chaguzi zijazo kwa gharama ya kudumaza maendeleo katika mikoa yao.

"Sina mpango wa kuchaguliwa tena ninapanga jinsi tutakavyobadilisha Kenya. Hiyo ndiyo dhamira yangu. Kuchaguliwa tena ni kwa mpango wa Mungu na mapenzi ya Wakenya. Kazi yangu si kupanga jinsi nitakavyorejeshwa- kuchaguliwa kazi yangu inabadilisha Kenya," alisema Rais huyo wa Kenya 

Wakati huo huo qliyekuwa Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ameishutumu serikali ya William Ruto kwa kumlaumu kila mara wanaposhindwa kutekeleza majukumu yao.

Rais huyo mstaafu amewataka waumini wa kanisa la Mwingi Full Gospel Church kukomesha siasa hasi huku akimsuta mrithi wake kwa kumlaumu kwa kushindwa kwa serikali yake na uchumi duni.

“Sitaki kusema mengi… si kwa sababu ninaogopa…niliacha kuogopa. Tumetishiwa, tumeambiwa mambo mengi. Kila mtu anaposhindwa husema ‘Oh! Serikali iliyopita,” amesema  Uhuru  #EastAfricaRadio