Jumanne , 20th Dec , 2022

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, amewataka wale wote wanaosema kwamba awamu yake inakopa sana, wasiache kusema kwamba hiyo ndiyo awamu yake inayojenga sana miundombinu.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan

Kauli hiyo ameitoa hii leo Desemba 20, 2022, mara baada ya kushuhudia sherehe ya utiaji saini mkataba wa SGR LOT 6 kipande cha Tabora hadi Kigoma, unaotarajiwa kukamilika katika kipindi cha miezi 48.

"Wanaosema awamu hii imekopa sana waseme pia ndiyo awamu iliyojenga sana, wasijifanye kama wanaume wa kiislamu Qur'an imewaambia kuoa wanne ruksa lakini hawamalizi aya, ruhusa lakini inafuatiwa na nini?, sasa wanasema awamu hii imekopa sana lakini imefanya nini? hawafiki huko," amesema Rais Samia