Jumatatu , 13th Sep , 2021

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, amefanya mabadiliko madogo kwenye Baraza la Mawaziri akiwateua January Makamba, Dkt. Stergomena Tax, Prof. Makame Mbarawa, na Dkt. Ashatu Kijaji.

Mbunge wa Bumbuli January Makamba ambaye ameteuliwa kuwa Waziri wa Nishati

Kwa mujibu wa taarifa ya Ikulu iliyotolewa jana Septemba 12, 2021, Rais Samia amemteua Mbunge wa Bumbuli January Makamba kuwa Waziri wa Nishati, akichukua nafasi ya Merdard Kalemani ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

Aidha, Rais amemteua Dkt. Ashatu Kijaji kuwa Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari akichukua nafasi ya Dkt. Faustine Ndugulile ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

Dkt. Ashatu Kijaji

Pia amemteua Dkt. Stergomena Tax kuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, akichukua nafasi ya iliyoachwa na Marehemu Elias Kwandikwa.

Dkt. Stergomena Tax

Naye Prof. Makame Mbarawa ameteuliwa kuwa Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi akichukua nafasi ya Mhandishi Dkt. Leonard Chamuriho ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

Prof. Makame Mbarawa

Wakati huo pia Rais Samia amemteua Dkt. Eliezer Feleshi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali akichukua nafasi ya Prof. Adelardus Kirangi ambaye ameteuliwa kuwa Balozi.

Dkt. Eliezer Feleshi

Viongozi hao wote walioteuliwa jana wataapishwa leo katika Ikulu ya Chamwino Jijini Dodoma.