Jumanne , 10th Sep , 2019

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, ametoa onyo kali kwa walimu wenye tabia ya kuwachezea wanafunzi na kuwataka wazingatie maadili ya kazi, kwani kazi ya ualimu inafanywa na watu wenye heshima.

Kulia ni Waziri wa Elimu Riziki Pembejuma, Katikati Rais Shein na pembeni ni Mwanafunzi aliyefanya vizuri.

Hayo ameyabainisha wakati wa hafla fupi ya kuwapongeza wanafunzi wa kidato cha sita waliofanya vizuri katika mtihani wa Taifa katika masomo ya Sayansi na Sanaa, Ikulu ya mjini Zanzibar.

''Wako baadhi ya walimu wanawaharibia walimu wengi wenye sifa nzuri, kwakuwa wao wako wachache, wakifanya hivyo wanawapunguzia ari na kasi na heshima katika kuwasomesha watoto wetu, wale Walimu waharibifu wanawadhalilisha vijana wetu pamoja na kina Mama'' amesema Rais Shein.

Aidha Dkt Shein ameongeza kuwa, Serikali yake itahakikisha inaendelea na utaratibu wa kuwapa ufadhili wa masomo ya Vyuo Vikuu wanafunzi bora wa kidato cha sita,  ambapo kwa mwaka huo imetoa ufadhili kwa wanafunzi 60 ikilinganishwa na mwaka jana ikiwa kama motisha kwa wengine kuongeza juhudi katika masomo.