Jumatatu , 6th Feb , 2023

Mkuu wa mkoa wa Tanga, Omary Mgumba amefafanua kuwa sababu za kuwasimamisha kazi Mganga mkuu wa halmashauri ya mji Korogwe, Salma Swedi na Mganga Mfawidhi wa hospitali ya wilaya ya Korogwe, Magunga Dkt. Heri Kihwale ni kutokana na kuchelewa kufika hospitalini kuwahudumia majeruhi

Akizungumza katika kipindi cha Supa Breakfast kinachorushwa na EARADIO Mgumba amesema, si kwamba watumishi hao walichelewa kufika eneo la ajali kama ilivyosemekana hapo awali.

Ajali hiyo ilitokea majira ya saa 4 na nusu usiku wa Februari tatu mwaka huu ambapo watumishi hao walifika hospitalini saa kumi kasorobo alfajiri ya Februari nne.

" Wanaishi jirani na hospitali na walikua wa kwanza kupokea taarifa lakini hawakuja mpaka mkuu wa wilaya ya Lushoto Kalist Lazaro ametoka umbali wa kilomita zaidi ya 70 amefika lakini wao bado,ajali imetokea saa 4 na nusu usiku wao wamefika hospitali saa kumi kasoro alfajiri." amesema mgumba