Jumamosi , 30th Apr , 2016

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Bw Jordan Rugimbana amewataka waajiri wa Mkoa Dodoma kuwaruhusu wafanyakaz

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Bw Jordan Rugimbana amewataka waajiri wa Mkoa Dodoma kuwaruhusu wafanyakazi wao kuhudhuria kwenye sherehe za siku ya Mei mosi kwani hiyo ni siku yao muhimu ya kujadili mambo mbalimbali yanayowahusu.

Bw Rugimbana ameitoa kauli hiyo kuelekea siku ya wafanyakazi duniani itakayoadhimishwa kitaifa Mkoani Dodoma na kuongeza kuwa kumnyima ruhusa mfanyakazi ni sawa na kumnyima haki yake ya msingi .

Aidha amewatajka wakazi wa mkoa wa Dodoma kuwa watulivu wakati wa kuadhimisha siku hiyo na kusiwepo na fujo zozote katika viwanja vitakapofanyika maadhimisho ya Meimosi.