
Wakizungumza mara baada ya kivuko hicho kukabidhiwa baadhi ya wananchi wamesema kivuko hicho kitawapunguzia adha ya usafiri kufuatia kivuko kilichopo hivi sasa cha Mv Kome 11 kutokidhi mahitaji huku wakiiomba serikali kuendelea na maboresho ya kivuko hicho ili wasinyeshewe na mvua na kupigwa na jua pindi wanapokuwa wanakitumia
‘Kipindi tunavuka kivho kilikuwa hakina shida sana labda kwa vile wametuletea kivuko kingine itakuwa ni fundisho kwa vivuko vingine na magari yatakayokuwepo yote yatavuka lakini bado kivuko hiki hakitutoshi tulitegemea wananchi wa kome tupate kivuko ambacho tukivuka hatulowani na mvua wala kupigwa na jua’
Meneja wa wakala wa ufundi na umeme mkoa wa Mwanza TEMESA Aloyce Ndunguru amesema kivuko cha Mv Sabasaba kimekarabatiwa kwa Zaidi ya shilingi milioni mia mbili nakina tani 85 na kinatarajiwa kubeba abiria 330, magari madogo 10 kwa wakati mmoja
‘Kivuko cha mv sabasaba kitapatia wananchi wa wilaya ya Sengerema uhakika wa usafiri na kitaunganisha wananchi wa visiwa vya kome na Nyakariro hivyo kukuza uchumi wao na kuwezesha kupata huduma mbalimbali kwa haraka na wakati kwahiyo kivuko cha Mv Sabasaba kimekarabatiwa tu kusaidiana na kivuko cha Kome two kwa kutoa huduma hapa lakini kivuko kipta kipo’
Akiwa kwenye makabidhiano ya kivuko hicho mbunge wa jimbo la Buchosa Erick Shigongo akasema kukarabatiwa kwa kivuko hicho kunaleta matumaini mapya kwa wakazi hao na kuwataka kusubiri kivuko kingine kipya
‘Nikasema Pamoja na kwamba tunauhakika kivuko kikibwa zaidi kinakuja na mkataba umeshainiwa na mkandarasi ameshapewa tayari bilioni mbili naomba kivuko kingine kitangulie kwanza angalau tupate mboga ya subuh na mchana ya jioni inakuja nikapambana kutafuta kivuko hiki nikakipata’