Jumatano , 14th Oct , 2015

Mkurugenzi la Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu NIMR DR. Mwela Malecela ameitaka Serikali kuongeza bajeti ya Utafiti ambayo kwa sasa ni asilimia moja tu ya bajeti ya nchini.

Mkurugenzi la Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu NIMR DR. Mwela Malecela.

Akizungumza na waandishi leo Dar es salaam katika kongamano la 29 la watafiti Dr Malecela amesema kuwa utafiti unahitaji fedha za kutosha na hivyo kuwataka wadau wa ndani pia kusaidia kufadhili tafiti kwa wafadhili wa nje huwa na masharti katika maeneo wanayoyataka wao tofauti na uhitaji wa nchini.

Dr Malecela ameongeza kuwa wananchi hawana sababu ya kwenda kutibiwa nje ya nchi kwani hospital zetu za rufaa zina uwezo wa kutibu maradhi makubwa kama moyo.

Kansa, kwa upande wate Profesa Morha Flanklini toka KCMC ambaye amepata tuzo ya mtafiti bora wa muda wote amewataka Wasomi vijana kupenda kufanya utafiti kwa maendeleo ya nchi.