
Wanafunzi
Wakizungumza na EATV hii leo Novemba 28, 2022, Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Yusuph Makamba Mahuvi Mapembe, amesema shule hiyo mwaka jana iliandikisha watoto 316 huku kwa mwaka huu mpaka sasa ni watoto 169 pekee wameandikishwa, huku shule ya msingi Mpakani ikiwa imeandikisha watoto 100 mpaka sasa lakini lengo likiwa ni kufikia wanafunzi 200.
Nao baadhi ya wazazi waliofika kuandikisha watoto wao kujiunga na darasa la kwanza wamesema, katika uandikishaji wa watoto wao changamoto kubwa waliyokutana nayo ni kukosa vyeti vya kuzaliwa vya watoto wao jambo lililowalazimu kuchelewa kuwaandikisha.
Kwa upande wake mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Maguruwe Peter Siro, iliyopo shule ya msingi Yusuph Makamba amesema wanaanza kupita nyumba hadi nyumba kuwabaini wazazi ambao wana watoto wenye umri wa kwenda shule lakini bado hawajawapeleka kuwaandikisha ili wawachukulie hatua za kisheria kama serikali ilivyowaelekeza.