
Ni wanaume kwa wanawake wakiwa katika hali ya utayari wakionesha madaha ya namna walivyo jiimarisha katika suala la ulinzi na usalama kupitia jeshi la jadi sungusungu.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Tabora wakati akizungumza na jeshi hilo la jadi amewambia hawapaswi kutumia nguvu zenye madhara makubwa kwa wahalifu ikiwemo kuua pindi wanapo wakamata.
Kamanda amesema suala la ulinzi na usalama ni jukumu la kila mwananchi kwa mujibu wa sheria .