Taarifa zaidi juu ya kifo cha msanii Godzilla

Jumatano , 13th Feb , 2019

Msanii wa hip hop nchini, Godzilla, amefariki dunia alfajiri ya leo nyumbani kwake baada ya kuugua ghafla.

Msanii Godzilla

Mtu wake wa karibu ameeleza kuwa presha ilishuka na sukari ilipanda pamoja na kuumwa na tumbo.

Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana, Godzilla amefariki dunia ghafla nyumbani kwao Salasala jijiji Dar es Salaam. Mwili umehifadhiwa katika Hospitali ya Jeshi ya Lugalo.

Kwa mujibu wa Wauguzi wa Hospital ya Lugalo, wamesema Godzilla aliletwa hapo akiwa ameshafariki, hivyo wamehifadhi mwili tu.

Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) pia limeonesha kuguswa na kifo cha msanii huyo, ambapo kupitia katika ukurasa wa Istagram wa baraza hilo, limeandika,

Historia fupi

Jina lake kamili ni Golden Jacob Mbunda, alizaliwa Januari 5, 1988 mkoani Morogoro. Alitambulika katika tasnia ya muziki kwa wimbo wake ulioitwa 'Salasala', ambao pia unatambulisha mtaa wake aliokuwa akiishi.

Tutakuletea taarifa zaidi kadri zitakapotufikia.