Alhamisi , 17th Nov , 2016

Serikali ya Tanzania imesema itahakikisha taasisi na mashirika yote ya umma yanajisajili na huduma za bima kutoka Shirika la Bima la Taifa kama mwongozo wa serikali unavyoelekeza sambamba na kuongeza mchango wa bima kwenye ukuaji wa uchumi.

Dkt. Philip Mpango - Waziri wa Fedha na Mipango

Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati akizindua Bodi ya Shirika la Bima la Taifa NIC na kwamba hatua hiyo itaisaidia kutunza na kulinda mali za umma dhidi ya majanga na ajali.

Israel Kauzora - Kamishna wa Bima

Kamishna wa Bima nchini Bw. Israel Kamuzora amesema kwa muda mrefu jamii imekosa elimu juu ya umuhimu wa bima kwenye uchumi na kwamba kuanzia sasa watahakikisha elimu inayafikia makundi yote na hasa jinsi bima inavyoweza kuchochea uchumi na ukuaji wa biashara.