Jumatatu , 11th Jul , 2016

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Kikanda na Kimataifa, Balozi Dk. Augustine Mahiga amewataka wadau mbalimbali wa maendeleo nchini kuendelea kuchangia sekta ya Elimu.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Kikanda na Kimataifa, Balozi Dk. Augustine Mahiga amewataka wadau mbalimbali wa maendeleo nchini kuendelea kuchangia sekta ya Elimu.

Balozi Mahiga ametoa wito huo leo jijini Dar es salaam wakati akizungumza na Jumuiya ya Umoja wa Mabohora waishio Tanzania ambao walikabidhi wizara hiyo madawati 105 kwa ajili ya shule mbalimbali nchini yenye thamani ya shilingi milioni 10.

Balozi Mahiga amesema uamuzi wa serikali kuanza kutoa elimu bure nchini umekua na faida kubwa kwa Watanzania kwa kuwa wazazi wengi wameamua kuwapelekea watoto wao shule hivyo ni wajibu wa kila Mtanzania kujitolea katika kuchangia Elimu ya taifa.