'Uchaguzi Tanzania sio kamari' - Bashiru Ally

Jumanne , 14th Jan , 2020

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Bashiru Ally ameseme maana halisi ya uchaguzi ni maamuzi ya umma, si kama ambavyo wamekuwa wakieleza kwa kupotosha kuwa uchaguzi ni namba.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Bashiru Ally

Ameyasema hayo alipokuwa akihutubia viongozi wa Mashina, Matawi, Kata na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Wilaya za Handeni na Kilindi mkoani Tanga.

Nimewasikia baadhi ya viongozi wa Vyama vya Siasa, wanasema uchaguzi ni namba, uchaguzi sio namba ni uamuzi wa umma, namba ni kitu cha baadaye, waambieni wanaosema uchaguzi ni namba waache kugeuza uchaguzi kama mchezo wa kamari au bingo"

Aidha Bashiru Ally amesema kuwa CCM inauona uchaguzi kama zoezi muhimu sana linalohusu uamuzi wa wananchi juu ya mustakabali wa taifa lao, uamuzi wa wananchi juu ya wananchi wenzao wanaofaa kuwaongoza kwa maendeleo yao.