Jumatatu , 9th Jan , 2023

Uganda inajiandaa kutangaza mwisho wa mlipuko wa Ebola baada ya kuibuka mwishoni mwa mwaka jana 

Wizara ya afya ya Uganda leo Jumatatu imesema kuwa ikiwa itafika kesho Jumanne bila kuripotiwa kwa kesi mpya ya Ebola basi Jumatano itatangaza kumalizika kwa ugonjwa huo nchini Uganda

Kwa mujibu wa Shirika la Afya duniani mlipuko wa ugonjwa wa Ebola unaisha ikiwa  hakuna kesi mpya kwa siku 42 mfululizo 

Tangu Uganda itangaze mlipuko huo Septemba 20/2022, taifa hilo limesajili visa 142 vilivyothibitishwa na vifo 56