
Waziri wa mambo ya nje wa Ukraine Dmytro Kuleba (kushoto) alipotembelea Senegal.
Waziri huyo Bwana Dmytro Kuleba, ameanza ziara barani Afrika .
Ubalozi wa Ukraine nchini Senegal umeshakutana na Waziri wa mambo ya nje wa Senegal Aissata Tall Sall na kutiliana saini mikataba mbalimbali ya kimashirikiano.
Waziri wa nje wa Ukraine Dmytro Kuleba yupo kwenye ziara inayoonekana kama majibizano ya kulitembelea bara ambalo tayari limeshatembelwa na maafisa wa ngazi za juu za Urusi , haswa likitembelewa Sergei Lavrov mwezi Julai mwaka huu, huku bara hilo liliwa na mipango ya kuwa mwenyeji wa mkutano wa Russia-Africa unaotarajiwa kufanyika nchini Ethiopia mwakani.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amekua akizitaka nchi za Afrika kulaani uvamizi wa Urusi kwenye nchi yake.