Ijumaa , 29th Aug , 2025

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameitaka Israel iachane na mpango wa kulidhibiti Jiji la Gaza. meyasema hayo wakati eneo hilo likikabiliwa na hofu ya janga la kiutu.

Kupitia ukurasa wake wa X, Katibu Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa aliandika kuwa tangazo la Israel kuhusu nia yake ya kulitwaa Jiji la Gaza linaashiria awamu mpya mbaya. 

Ameongeza kuwa hatua hiyo itawalazimisha maelfu ya raia kukimbia na kuzitumbukiza familia katika hatari kubwa. Itakumbukwa kuwa, Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, ameliamuru jeshi kulidhibiti Jiji la Gaza linaoaminiwa kuwa na takribani wakaazi milioni 1. 

Wakati huo huo, jeshi la Israel limesema leo kuwa limesitisha mapumziko ya  mchana yanayotoa nafasi ya kuwasilishwa kwa misaada katika jiji hilo na kudai kuwa eneo hilo ni hatari.