Jumatano , 5th Oct , 2016

Kampuni ya Uwekezaji ya UTT AMIS, imeanza kutoa huduma mpya ya kifedha inayowawezesha watu wenye kiasi kikubwa cha fedha kuwa na makubaliano ya kibiashara na kampuni hiyo kuhusu uwekezaji unaofaa kufanywa kwa kutumia fedha hizo

Mkurugenzi wa Masoko na Uhusiano wa UTT AMIS Bw. Daudi Mbaga

Huduma hiyo ni badala ya mtu kuziacha pesa hizo hizo zikae pasipo kutengeneza faida.

Mkurugenzi wa Masoko na Uhusiano wa UTT AMIS Bw. Daudi Mbaga, amesema huduma hiyo inafanana sana na ile ya custodianship inayotolewa kwa wawekezaji kwenye masoko ya mitaji na dhamana na kwamba itazuia uwezekano wa watu kukaa na kiasi kikubwa cha pesa pasipo kuzifanyia shughuli ya uzalishaji.

Bw. Mbaga amewataka wafanyabiashara kuchangamkia fursa hiyo hasa kutokana na rekodi nzuri iliyonayo UTT AMIS ambayo hutoa faida kubwa sambamba na kumwezesha mwekezaji kuchukua kiasi cha pesa alizowekeza ndani ya muda mfupi kuliko uwekezaji katika maeneo meingine.