Jumatano , 5th Oct , 2016

Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman amesema mfumo wa sasa wa kuandika mashauri kwa mkono umekuwa ukichelewesha uendeshaji wa mashauri .

Jaji Mkuu, Mohamed Chande Othman

Jaji Othman Chande ameyasema hayo leo jijini Dar es salaam wakati akiongea na waandishi wa habari kuhusiana na Ziara ya Jaji Mkuu wa Australia Kusini Mh. Christopher Kourakis ambaye yupo nchini kwa ziara ya siku tatu.

Jaji Chande amesema kutokana na changamoto hiyo wanaanzisha kada mpya ya wapiga chapa maalum wanaotumia mashine ili shauri likiwa linaendelea inapofika mchana nakala ya shauri hilo inakuwa tayari.

Jaji Chande ameongeza kuwa kwa kufanya hivyo kutaondoa changamoto hiyo ili kuwezesha haki kutendeka kwa wakati.