Jumatano , 20th Jul , 2016

SERIKALI imewataka wadau ,taasisi,sekta binafsi na asasi zote nchini kuhakikisha wanatumia takwimu za tafiti zinazofanywa ili kuboresha sera na mipango ya kupambana na utumikishwaji wa watoto nchini .

Hayo yamezungumza leo jijini Dar es salaamu na naibu waziri ofisi ya waziri mkuu sera bunge kazi vijana ajira na watu wenye ulemavu Mheshimiwa dokta ABDALAH POSSI wakati wa uzinduzi wa ripoti ya matokeo ya utafiti wa utumikishwaji wa watoto ncini kwa mwaka 2014 ambapo amesema kumekuwepo na dhana hasi kwa wadau nchini kuwa matumizi ya tafiti ni kwa ofisi za serikali na kuanza mtazamo mpya wa kuanza kutumia tafiti kama hizo kwa ajili ya kutunga sera na mipango ya baadae itakao toa suluhisho .

Takwimu zinaonesha kuwa watoto Milioni 4.3 wanatumikishwa katika kazi za Kilimo, Mifugo, Uvuvi pamoja na Madini nchini Tanzania kati ya watoto Milioni 15 hali inayochangiwa na kipato duni katika ngazi ya kaya ambapo 74.7% ya watoto kote nchini wanafanya kazi hatarishi.

Dokta POSSI ameongeza kuwa katika ripoti hiyo utafiti umebainisha kuwa utumikishwaji wa watoto nchini umebainisha kuwa kundi kubwa la watoto wanaotumikishwa ni wa umri wa miaka 5 mpaka 11ambapo ni watoto milioni 15 sawa na asilimia 59.6 likifuatiwa na watoto wenye umri wa miaka 14 mpaka 17 ambapo ni sawa na asilimia 24.6

Aidha dokta POSSI amesema serikali itaendelea na mapambano dhidi ya ajira kwa watoto nchini ili kutoa nafasi kwa watoto kwenda shule na kupata nafasi ya kujipatia elimu kupitia sera ya elimu bure.

Awali akizungumza kabla ya mheshimiwa naibu waziri mkurugenzi mkuu wa utafiti kutoka ofisi ya taifa ya takwimu NBS dokta ALBINA CHUWA amebainisha katika utafiti waliofanya umeonesha kuwa utumikishwaji wa watoto ni tatizo kubwa licha ya kupungua kwa silimia 3.1 ambapo utafiti wa mwisho kufanywa kwa mwaka 2006 ulionesha zaidi ya asilimia 31 ya watoto wamekuwa wakitumikishwa na kwa utafiti wa mwaka 2014 umebaini utumikishwaji kwa asilimia 28.8.