
Biashara ya Nyanya katika moja ya soko Dar es Salaam
Baadhi ya madalali wanaoshusha nyanya katika masoko mbalimbali wameiambia EATV kuwa bei imepanda kutokana na kiasi kidogo cha shehena ya nyanya kinachoingia sokoni hapo kwa sasa wanategemea nyanya kutoka kwa wakulima wa Arusha, Iringa na Makambako pekee.
Kwa upande wao baadhi ya wafanyabiashara wadogo wanaouza nyanya kupitia vipimo vya asili maarufu kama sado, wamesema kupanda kwa bei kumefanya biashara kuwa ngumu kwani wateja wamekuwa hawamudu ongezeko hilo la bei.