Ijumaa , 19th Feb , 2016

Wafugaji mkoani Arusha wamelalamikia ukosefu wa miundombinu rafiki katika mnada wa ng`ombe hali inayosababisha adha kubwa hasa wakati wa mvua kutokana na soko hilo kutokuwa na paa wala uzio .

Wafugaji wakiwa wananyeshwa mvua na mifugo yao Mkoani Arusha katika Mnada wenye miundo mbinu mibovu

Katika mnada huo nimeshuhudia mvua kubwa ikinyesha huku mifugo na watu wakinyeeshewa bila kuwa na sehemu ya kujihifadhi jambo ambalo linaathiri afya za wanyama na kukiuka haki za wanyama.

Frank Zablo ni Mfugaji ambaye hufika katika soko hilo kuuza mifugo anasema kuwa ng`ombe wakinyeshewa hubadilisha hali zao kiafya hivyo kupelekea bei kushuka wakiwa sokoni hvyo ameiomba serikali iwasaidie kujenga mnada wenye miundombinu bora.

Lemayan Mollel anaeleza kuwa licha ya soko hilo kuwa na manufaa kiuchumi kwa watu wenye miradi ya ufugaji katika kipindi cha mvua hali ya soko huwa mbaya.

Kwa upande wake mfanyabiashara ya mifugo katika soko hilo Mwangi Sandu ameitaka serikali ifanye maboresho katika soko hilo kwani wanapata adha kubwa ya kunyeshewa na mvua hali inayopelekea kusimama kwa shughuli kunakosababisha serikali kukosa mapato yake.

Tanzania ni kati ya nchi zinazoongoza kwa ufugaji barani Afrika inashika nafasi ya pili, serikali inapaswa kujenga miundombinu rafiki ili kuwezesha ufugaji bora na soko bora ambalo linaweza kuwawezesha wafugaji kufanya biashara na kunufaika.