Jumatatu , 16th Jun , 2014

Wajasiriamali nchini Tanzania wameaswa kuzalisha bidhaa zenye ubora badala ya kutengeza nakuziuza kwa wananchi wakati bado hazijapimwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS).

Afisa habari wa Shirika la viwango Tanzania - TBS Bi. Roida Andusamile (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa idara ya habari MAELEZO hivi karibuni.

Hayo yalisemwa na Ofisa habari wa Shirika la viwango Roida Anduamile wakati wa maonyesho ya wajasiriamali yaliyofadhiliwa na shirika la Viwanda Vidogo (SIDO).

Aidha alisema kuwa wajasiriamali 258 wamefikiwa na TBS na Kupimiwa ubora wa bidhaa zao nchi nzima, na kuwataka wengine kufika katika ofisi za Shirika hilo ili kukaguliwa mazingira wanayofanyia kazi kuhakiki kama kweli bidhaa zinazozalishwa zinaubora unaotakiwa.