Jumatano , 11th Mei , 2022

Jeshi la polisi Mkoani Mtwara, linawashikilia watu wawili na mmoja bado anatafutwa na jeshi hilo kwa tuhuma za kumbaka  kisha kumuua  Elizabet Steven Peter  (41) mkazi wa Kijiji cha Mkajamila wilaya ya Masasi Mkoani humo.

Kaimu Kamanda Jeshi la Polisi mkoani Mtwara, ACP Nicodemus Katembo

Akizungumza na waandishi wa Habari Mkoani hapo,  Kaimu Kamanda Jeshi la Polisi mkoani humo, ACP Nicodemus Katembo amesema, tukio hilo linadaiwa kufanyika, Mei 6 mwaka huu, ambapo inadaiwa   watuhumiwa hao walimbaka marehemu  na kisha kumvunja shingo kwa kile kinachodaiwa kuwa ni wivu wa mapenzi.

Aidha katika tukio lingine Polisi mkoani Mtwara wanafanya uchunguzi wa kifo cha  Hassan Mumwela, (35) mfanyabiashara na  mkazi wa Kijiji cha Namhi  Kata ya Libobe Wilaya ya Mtwara, baada ya  mfanyabiashara huyo, kuanguka ghafla na kupoteza maisha akiwa katika  eneo lake la biashara.