
Rais wa Jamhuri ya Muunganio wa Tanzania Samia Suluhu Hassan
Kauli hiyo ameitoa hii leo Agosti Mosi, 2022, mara baada ya kuwaapisha viongozi mbalimbali wakiwemo wakuu wa mikoa, makatibu tawala wa mikoa na wakuu wa mashirika, Ikulu ya jijini Dar es Salaam.
"Wengine wala mlikuwa hamjaapa tayari nina malalamiko yenu, chochote ulichokuwa unakifanya kajirekebishe, ili angalau basi upate miezi 6, 7, kwa sababu kama unafanya vibaya nilisema, sito-shout na mtu nitaondoa tu na kuweka mwingine," amesema Rais Samia